Masharti ya Matumizi ya Premise

Tarehe ya Kuanza Kutumika: 1 Aprili, 2024

Masharti ya matumizi yafuatayo (“Mkataba”) yanasimamia matumizi yote ya aplikesheni za Premise za vifaa vya mkononi (“Aplikesheni”), tovuti ya Premise “www.premise.com” (“Tovuti”) na lango la Premise au huduma nyingine za mtandaoni zinazotolewa na Premise (“Jukwaa”) na bidhaa pamoja na huduma zinazopatikana kwenye au kupitia Aplikesheni, Tovuti na Jukwaa (zikichukuliwa kwa pamoja Aplikesheni, Tovuti na Jukwaa, “Huduma”). Huduma inatolewa kwa kutegemeana na kukubali kwako, bila mabadiliko yoyote, na masharti yaliyomo ndani ya Mkataba huu pamoja na sheria, sera na taratibu zote zinazoweza kusambazwa kwenye Aplikesheni, Tovuti na Jukwa au zilizojumuishwa katika Kazi (Imefafanuliwa hapo chini). Ufikiaji wako pamoja na/au matumizi yako ya Huduma huonyesha kukubaliana kwako na Mkataba huu, hivyo kuunda makubaliano ya kisheria. Unapobofya “Nimekubali” kwenye Aplikesheni au Jukwaa, kitendo hicho pia huunda makubaliano ya kisheria na huonyesha kukubaliana kwako na Mkataba huu. Mkataba huu huenda ukaboreshwa mara kwa mara, kama itakavyolezewa zaidi hapo chini.

Tafadhali tumia muda wa kutosha kusoma kwa makini Mkataba huu. Unaweza tu kutumia Huduma kwa niaba ya kampuni kwa kupewa mamlaka yaliyotolewa mapema na kampuni hiyo na ambayo yako katika maandishi. Wewe, au Kampuni ambayo unatumia Huduma kwa niaba yake, mtarejelewa ndani ya Mkataba huu kama “wewe,” “Kampuni yako” au “Mtumiaji.” Huduma hii inamilikiwa na kuendeshwa na Premise Data Corporation (“PDC”). Iwapo utakuta sehemu yoyote ndani ya Mkataba huu ambayo inakuchanganya, tafadhali tuma barua pepe kwa PDC kupitia: [email protected].

MASHARTI HAYA YANAJUMUISHA KIFUNGU CHA LAZIMA CHA USULUHISHI WA MTU BINAFSI NA HATI YA KUSAMEHE MADAI YA KESI YA KIKUNDI/YENYE WAAMUZI AMBAYO HUTAKA MATUMIZI YA USULUHISHI WA MTU BINAFSI ILI KUTATUA TOFAUTI, BADALA YA KESI ZA MAKUNDI AU ZENYE WAAMUZI.

ENDAPO HUKUBALIANI NA SHERIA NA MASHARTI YOTE YALIYOMO KATIKA MKATABA HUU, USITENGENEZE AKAUNTI NA USITUMIE AU KUFIKIA HUDUMA.

MASHARTI YA UMRI

Huduma inaweza kutumiwa tu na watu walio na umri usiopungua miaka 18 au walio na umri wa mtu mzima katika maeneo au nchi ambapo mtu huyo anaishi wakati wa kutengeneza akaunti ili kutumia Huduma, na mahali ambapo mtu huyo anakamilisha Kazi (Imefafanuliwa hapo chini).

FARAGHA

Sera ya Faragha ya PDC inapatikana kwenye Tovuti na Jukwaa (Sera ya Faragha) na imejumuishwa humu ndani kupitia rejeo hili. Pia, Sera ya Faragha (https://tos.premise.com/privacy-policy/) inapatikana kupitia Aplikesheni. PDC inakuhimiza usome Sera ya Faragha kwa umakini. Kukubaliana kwako na Mkataba huu huonyesha kukubaliana kwako na Sera ya Faragha, kama itakavyoboreshwa mara kwa mara.

MASHARTI YA KUFIKIA NA KUTUMIA

Kama hitaji la kupokea stahiki yoyote chini ya Mkataba huu, Mtumiaji anahakikisha kwamba yeye wala mtu mwingine yeyote anayehusika na Mtumiaji kutoa huduma chini ya Mkataba huu:

    1. hakai au haishi nchini Kuba, Irani, Korea ya Kaskazini, Sudani, Siria, au kanda ya Krimea ya Ukraini/Urusi, au nchi yoyote au eneo lililopo chini ya vikwazo kamili vilivyowekwa chini ya mipango ya vikwazo vya Idara ya Hazina ya Marekani (Taarifa kuhusu mipango hiyo inapatikana hapa: Mipango ya Vikwazo na Taarifa za Nchi); au
    2. hakabiliwi na vikwazo vya kibiashara vilivyowekwa na Serikali ya Marekani, ikijumuisha, lakini si tu, vikwazo vilivyowekwa na Idara ya Hazina ya Marekani chini ya mipango ya vikwazo, pamoja na Idara ya Biashara na Umoja ya Marekani chini ya sheria za udhibiti wa biasharanje za Marekani. Orodha ya kiujumla ya watu waliowekewa vikwazo hivyo inapatikana hapa: Orodha ya Uchunguzi Iliyounganishwa.

PDC huchukulia suala la kuzuia udanganyifu na utii wa sheria kwa uzito mkubwa. Kama hitaji la kujisajili na kukamilisha Kazi (Imefafanuliwa hapo chini), Mtumiaji anakiri na kukubali kwamba PDC inaweza kufanya uchunguzi wa kina wa kiusalama na kumhusu, kama itakavyoona inafaa na kwa busara zake yenyewe.

Mtumiaji anahakikisha na kuthibitisha kwamba:

    1. Mtumiaji hajatambuliwa kwenye orodha yoyote ya watu au vikundi ambavyo vimepigwa marufuku kama vile, orodha iliyohifadhiwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, serikali ya Marekani (ikiwa ni pamoja na Orodha ya Wananchi Maalumu ya Idara ya Hazina ya Marekani na Orodha ya Wakwepaji wa Vikwazo vya Kigeni), Umoja wa Ulaya (EU) au nchi zake wanachama, na serikali ya nchi yako endapo upo nje ya Marekani na EU; na 
    2. Mtumiaji hamilikiwi wala kudhibitiwa na, au kufanya kazi kwa niaba ya, mtu au chombo kilichomo kwenye orodha yoyote iliyoelezwa hapo juu; na
    3. Mtumiaji hana vikwazo vya kumkwamisha kupokea malipo kutoka, au kufanya huduma kwa, PDC chini ya sheria na kanuni zinazohusika nchini Marekani na EU na/au sheria nyinginezo zinazohusika; na
    4. Mtumiaji haungi mkono wala kushiriki kikamilifu katika shughuli za kigaidi; na
    5. Mtumiaji hatatoa msaada wowote (wa kifedha au usio wa kifedha) kwa mtu au shirika lolote, ikijumuisha bila ukomo watu na taasisi zilizobainishwa na Wizara ya mambo ya nchi za nje chini ya Amri ya Serikali nambari 13224, linalojihusisha na shughuli za kigaidi kutokana na kupata malipo yoyote ya kifedha kutoka kwa uhusiano wao na PDC; na
    6. Mtumiaji, iwe kwa kutenda kwa niaba yake binafsi au kwa niaba ya kampuni, ana umri usiopungua miaka 18 (au ametimiza umri wa kisheria wa mtu mzima ndani ya eneo ambalo Mtumiaji anaishi na anakamilisha Kazi (Imefafanuliwa hapo chini)), Mtumiaji anaruhusiwa kisheria kutumia Huduma na atachukuwa wajibu kamili kwa kuchagua na kutumia Huduma.

Kushindwa kutekeleza masharti yoyote yaliyoelezwa hapo juu huenda yakasababisha uwajibikaji wa kisheria kwa PDC au wahusika wengine, au huweza kuwa kosa la kisheria. Aidha, kushindwa kutekeleza masharti yaliyoelezwa kutasababisha kukomeshwa kwa haraka Mkataba huu, kupoteza stahiki zozote ambazo zinaweza kuwa zinadaiwa kutokana na kukamilisha Kazi (Imefafanuliwa hapo chini) kama ilivyoruhusiwa na sheria, usuluhishi, dai au taratibu nyinginezo za kisheria kwa mujibu wa masharti ya Mkataba huu, na taarifa kwa mamlaka husika.

Kwa mujibu wa masharti ya Mkataba huu na kufuatwa kwake au kutiliwa maanani na mtumiaji, PDC itampatia Mtumiaji Huduma – kwa matumizi ya Mtumiaji pekee kulingana na nyaraka zote na maelekezo mengine yaliyoandikwa na PDC (ikiwa ni pamoja na, bila kikwazo chochote, kama vitavyochapishwa na PDC kwenye Tovuti, kusambazwa kupitia Aplikesheni, au kubainishwa kwenye maelezo ya Kazi). 

Mtumiaji anakiri kwamba Huduma inaweza kuwa na vipindi vya kutokuwepo hewani kutokana na matengenezo na masasisho. Baada ya kufanyika kwa masasisho hayo, huenda ukakuta vipengele vipya vimeongezwa au vipengele vilivyo kuwepo kuondolewa.

Mtumiaji atakuwa na jukumu la kupata na kudumisha vifaa vyovyote au huduma zinazohitajika kuunganisha na kufikia Huduma, ikiwa ni pamoja na (lakini si hizi pekee) ufikiaji wa intaneti, huduma ya Wi-Fi, huduma za ujumbe mfupi za papo kwa hapo, modemu, maunzi ngumu, maunzi tepe, na huduma za simu za ndani au za kimataifa. Mtumiaji atakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa vifaa au huduma zinaweza kutumika na Huduma.

Mtumiaji atawajibika kwa gharama zote zinazohusiana na Huduma pamoja na kukamilisha Kazi (Imefafanuliwa hapo chini), ikijumuisha (lakini si hizi pekee) gharama za vifurushi vya intaneti, gharama za kufikia mtandao, gharama za SMS na ujumbe wa papo kwa hapo, gharama za huduma ya mawasiliano ya simu bila waya, maboresho ya programu na vifaa, na gharama za utumaji wa data.

Ikiwa Mtumiaji anaendesha chombo cha usafiri, pikipiki, skuta au aina nyingine ya usafiri binafsi (zote kwa pamoja, “Chombo cha Usafiri”) wakati anakamilisha Kazi (Imefafanuliwa hapo chini), Mtumiaji ataendesha Chombo cha Usafiri hicho kwa usalama na hatatumia simu wala kifaa chochote kingine wakati Chombo cha Usafiri hicho kipo katika mwendo. Pia, Mtumiaji atakuwa na kiwango cha chini cha bima cha chombo cha usafiri kinachohitajika kisheria au bima nyingine ya dhima inayofaa au, ikiwa hakuna kiwango cha chini cha bima kinachohitajika kisheria katika eneo alilopo, basi kiwango chochote cha bima ya chombo cha usafiri au bima nyingine ya dhima inayoweza kufidia upotevu au majeraha yaliyosababishwa na Mtumiaji. Mtumiaji anakiri kuwa PDC haiwajibiki kwa upotevu au majeraha yoyote yatakayosababishwa na Mtumiaji akiwa anakamilisha Kazi na, kama ilivyoelezewa katika sehemu ya Fidia hapo chini, Mtumiaji ataifidia PDC dhidi ya madai ya watu wengine yanayotokana na matendo ya Mtumiaji wakati akikamilisha Kazi.

KAZI, STAHIKI, KIWANGO CHA CHINI CHA MALIPO NA MAKATAA, ADA NA KODI

Watumiaji wanaopakua Aplikesheni wanaweza kujisajili ili kukamilisha utafiti, kuwasilisha video, picha za skrini, picha au rekodi mbalimbali zinazowahusisha wao na/au vitu wanavyoviona, au kufanya miradi mingineyo (“Kazi”). Mahitaji ya kila Kazi, ikiwa ni pamoja na shughuli inayopaswa kukamilishwa, muda, mahali na aina ya taarifa inayohitajika (kama vile, jibu la utafiti, taarifa zilizoonekana katika eneo, picha, picha ya skrini au video), hubainishwa kwenye notisi ya Kazi na zimewekwa hapa kama rejeleo. Vilevile, notisi ya Kazi inaweza kubainisha taarifa za ziada juu ya ukusanyaji, matumizi au ushiriki wa data, hivyo kujazilia Sera ya Faragha iliyojumuishwa humu ndani. Notisi ya Kazi pia inabainisha stahiki zipi zinaweza au kutoweza kuongezwa katika salio la Mtumiaji baada ya kukamilisha na kukubaliwa kwa wasilisho la Kazi. Stahiki hupatikana kwa kufuata masharti ya Mkataba huu pindi Kazi inavyokamilishwa kwa kufuata Mkataba huu na kuthibitishwa/kukubaliwa (Kukamilishwa kwa Kazi). Hakuna uhusiano wa mwajiri na mwajiriwa utakaoanzishwa kwa kujisajili au kukamilisha Kazi.

Mchakato wa Kutoa Malipo na Kiwango cha Chini cha Malipo. Watumiaji wanapaswa kuchagua njia ya kupokea stahiki zao kutoka machaguo yanayopatikana kwenye Aplikesheni katika eneo wanaloishi na kukamilisha Kazi. PDC hutumia huduma kutoka kwa wahusika wengine ili kuwezesha mchakato huo kama vile, Mobile Top-Up, PayPal, Coinbase na Payoneer. Huduma zinazotumika kudhibiti mchakato kwa kawaida huwa na kiwango cha chini cha malipo. Ikimaanisha, hutoweza kutoa malipo hadi ukamilishe Kazi za kutosha ili ufikishe kiwango cha chini. Kiwango hicho kimebainishwa ndani ya Aplikesheni pindi unapojisajili kwa ajili ya huduma ya malipo na viwango hivi huenda vikatofautiana baina ya nchi na nchi. Viwango vya kutoa malipo huweza kubadilika kutokana na Mtoa huduma au PDC. Unahimizwa kuangalia kiwango cha kutoa pesa kinachoonekana kwenye Aplikesheni mara kwa mara ili utambue badiliko lolote.

Ukomo wa Kutoa Malipo. Kwa Kazi yoyote itakayokamilishwa tarehe 1 Aprili, 2022, au baada ya hapo, Watumiaji wanapaswa kutoa stahiki zao ndani ya miezi sita ya kupokea notisi ya Kukamilishwa kwa Kazi (“Kipindi cha Kutoa Malipo”). Kwa Kazi yoyote iliyokamilishwa kabla ya tarehe 1 Aprili, 2022, muda wa kutoa malipo ulikwisha tangu tarehe 31 Machi, 2023 (“Kipindi Kilichoongezwa cha Kutoa Malipo”). Kushindwa kutoa malipo katika Kipindi cha Kutoa Malipo au Kipindi Kilichoongezwa cha Kutoa Malipo huenda kukakusababishia kulipa ada, kupoteza stahiki au yote mawili kwa pamoja, kama ilivyoelezwa ndani ya Mkataba huu. Watumiaji wanaweza kufuatilia muda wa stahiki unaopatikana kupitia historia zao za Kazi kwenye Aplikesheni na kutambua tarehe ya Kukamilishwa kwa Kazi na kiasi cha stahiki cha Kazi, kama kipo.

Ada kwa ajili ya Utoaji Malipo Uliochelewa. Endapo Mtumiaji yeyote atashindwa kutoa stahiki zinazopatikana kabla ya muda wake kuisha kulingana na Kipindi cha Kutoa Malipo au Kipindi Kilichoongezwa cha Kutoa Malipo (“Malipo Yaliyopita Muda Wake”), PDC inaweza kutoza ada ya US$1 kwenye Malipo Yaliyopita Muda Wake, kwa kila mwaka ambao Malipo Yaliyopita Muda Wake hayakutolewa. 

Hali Zisizofuata Makataa ya Kutoa Malipo. Ikiwa Mtumiaji hawezi kutoa malipo kutokana na PDC kutokufanya Kazi za kutosha zipatikane ndani ya eneo ambalo Mtumiaji alitengeneza akaunti ya PDC ya Mtumiaji ili imuwezeshe Mtumiaji kufikisha kiwango cha chini cha kutoa malipo kilichowekwa na watoa huduma wa malipo wengine au PDC ndani ya vikomo vya muda vinavyohusika (Kipindi cha Kutoa Malipo au Kipindi Kilichoongezwa cha Kutoa Malipo), Mtumiaji anaweza kuwasiliana na PDC kupitia: [email protected] ili aombe unafuu wa makataa ya kutoa malipo na/au ada. PDC inaweza, kwa busara zake, (1) kuondoa ada kwa kipindi chochote cha muda au (2) kufanya utaratibu wa Mtumiaji kulipwa kupitia ACH au hamisho la pesa kupitia benki au njia nyingine ya malipo itakayochaguliwa na PDC ikiwa Mtumiaji atatoa maelezo ya kutosha ili PDC iweze kuthibitisha utambulisho wa Mtumiaji na taarifa za akaunti za kutosha ili kuwezesha uhamishaji wa malipo hayo kufanyika kupitia sarafu iliyobainishwa katika Kazi.

Iwapo Mtumiaji anaamini kuwa PDC imefanya makosa katika stahiki za Mtumiaji, Mtumiaji anapaswa kuwasiliana na PDC kupitia: [email protected] kwa usaidizi.

Mtumiaji si mwajiriwa wa PDC. Mtumiaji anawajibika na kodi zote zinazohusiana na matumizi ya Huduma na stahiki zozote zilizopokelewa baada ya kukamilisha Kazi. PDC inaweza kutuma nyaraka za kodi za Mtumiaji, kama vile “Form 1099” ya nchini Marekani.  

MAREKEBISHO, MABORESHO NA USIMAMISHAJI

PDC inaweza kubadilisha, kusimamisha au kusitisha Huduma wakati wowote, ikiwa ni pamoja na kipengele, hifadhidata au maudhui yoyote. PDC inaweza pia kuweka mipaka kwa baadhi ya vipengele vya Huduma au kuzuia Mtumiaji kufikia sehemu ya au Huduma nzima bila notisi au dhima.

PDC inahifadhi haki, kwa busara zake binafsi, za kubadilisha Mkataba huu muda wowote kwa kuchapisha notisi kwenye Tovuti, Jukwaa au kupitia Aplikesheni, au kwa kumtumia Mtumiaji notisi kupitia barua pepe au kama barua. Mtumiaji atakuwa na jukumu la kusoma na kuelewa mabadiliko hayo. Matumizi ya Huduma na Mtumiaji baada ya arifa kama hiyo huonyesha Mtumiaji kukubaliana na sheria na masharti ya Mkataba huu kama yalivyobadilisha.

APLIKESHENI, MAUDHUI YA TOVUTI NA JUKWAA NA HAKI ZA UVUMBUZI

Mtumiaji anakubali kuwa maudhui yote, kama alama za biashara, maandishi, grafu na alama zinazoonekana, data, takwimu, vipimo, nembo, aikoni za vitufe, picha vipande vya sauti, vipakuliwa vya kidijitali, taarifa zilizokusanywa, nyenzo, maunzi laini na nyinginezo (zote kwa pamoja, “Maudhui”) yanayotolewa na PDC kupitia Huduma au vinginevyo kutolewa na PDC kupitia Aplikesheni, Tovuti au Jukwaa hulindwa na hakimiliki, alama za biashara, alama za huduma, haki za uvumbuzi, siri za kibiashara au haki na sheria nyinginezo za umiliki. Isipokuwa kama imeidhinishwa kwa maandishi na PDC, Mtumiaji anakubali kutouza, kukabidhi leseni kwa wengine, kukodi, kubadilisha, kusambaza, kunakili, kuzalisha, kutangaza, kuonyesha hadharani, kuchapisha, kutengeneza, kuhariri au kuunda kazi zinazotokana na Maudhui hayo, na anakubali kutotumia alama ya biashara ya PDC isipokuwa kama anaitaja PDC au bidhaa na huduma zake. Mtumiaji anaweza kuchapisha au kupakua idadi inayoeleweka ya nakala za Maudhui kutoka kwenye Aplikesheni, Tovuti, au Jukwaa kwa ajili ya matumizi binafsi ya Mtumiaji ya kujipatia taarifa ikiwa tu, Mtumiaji atahifadhi hakimiliki zote na matangazo mengine ya wamiliki yaliyomo ndani ya ala hizo. Kitendo cha kuzalisha, kuiga au kusambaza Maudhui, nyenzo au vipengele vya kubuni vyovyote kwenye Aplikesheni, Tovuti au Jukwaa kwa kusudi lolote bila kibali cha maandishi cha PDC kinapigwa marufuku makali.

Matumizi ya Maudhui kwa madhumuni yoyote yasiyoruhusiwa kinaga ubaga katika Mkataba huu ni marufuku. Haki zozote zisizopewa wazi hapa zimehifadhiwa.

Isipokuwa kama ilivyobainishwa humu, PDC pekee (na watoa leseni wake, inapofaa) itahifadhi haki zote za uvumbuzi zinazohusiana na Huduma. Maudhui yote yaliyomo kwenye Aplikesheni, Tovuti au Jukwaa ni mali ya PDC au wasambaza Maudhui wake. Mkusanyiko wa Maudhui yote ndani ya Aplikesheni, Tovuti au Jukwaa ni mali ya PDC pekee.

Mkataba huu si mauzo na hauwasilishi haki zozote za umiliki ndani au zinazohusiana na Huduma, Maudhui yoyote au haki zozote za uvumbuzi.

MAUDHUI YA MTUMIAJI

Mtumiaji anakiri na kukubali kwamba Mtumiaji akichangia Maudhui katika Aplikesheni, Tovuti au Jukwaa, au kuchangia Maudhui yanayohusiana na Kazi (“Maudhui ya Mtumiaji”), PDC (na warithi wake pamoja na atakaowapa mamlaka) hupewa nafasi isiyo ya kipekee, duniani kote, inayodumu, isiyoweza kubadilishwa, bila malipo na ya kuhamishika kutumia kikamilifu Maudhui ya Mtumiaji (ikiwa ni pamoja na haki zote zinazohusiana na uvumbuzi), kwa madhumuni yoyote, na kuruhusu wengine kufanya hivyo (ikijumuisha watu wengine waliyoishirikisha PDC kudhibiti Kazi au wateja wa watu hao). Mtumiaji anaachilia haki zozote za kimaadili kwa au haki za kujulikana katika Maudhui ya Mtumiaji, ikiwa zipo, na haki yoyote ya kutambuliwa ambayo Mtumiaji anaweza kuwa nayo. PDC ina haki ya kuondoa Maudhui yoyote ya Mtumiaji kutoka kwenye Aplikesheni, Tovuti au Jukwaa wakati wowote, kwa sababu yoyote (ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, baada ya kupokea madai au malalamishi yanayohusiana na Maudhui ya Mtumiaji kutoka kwa watu wengine au mamlaka), au bila sababu yoyote ile.

Mtumiaji anawakilisha na kuhakikisha kwamba (i) Mtumiaji ana haki, mamlaka na uwezo wote wa kuchangia Maudhui yote ya Mtumiaji kwa PDC na Aplikesheni, Tovuti na Jukwaa, na kutoa leseni iliyotolewa awali na haki pamoja na hati za kusamehe madai (ii) Maudhui ya Mtumiaji  hayakiuki wala kuvunja haki za mtu mwingine na/au kuifanya PDC, wafanyakazi wake, makontrakta, maafisa, wakurugenzi, mawakala au washirika, au wahusika wengine ambao huishirikisha PDC kusimamia Kazi (pamoja na wateja wao) kuwajibika kisheria (iii) Maudhui ya Mtumiaji na kukamilishwa kwa Kazi yoyote hakutakuwa na mgongano wowote wa wajibu Mtumiaji alionao na wahusika wengine, na (iv) Maudhui ya Mtumiaji wala Mawasilisho hayatakiuka sheria au kanuni zozote.

Kama ilivyoelezewa katika sehemu ya Faragha hapo juu, ikiwa Maudhui ya Mtumiaji yanajumuisha taarifa binafsi, basi taarifa hizo zitafanyiwa kazi na PDC kwa mujibu wa Sera ya Faragha.

Mtumiaji anakiri na kutoa ridhaa yake, kwamba taarifa zozote binafsi zilizopo kwenye Maudhui ya Mtumiaji: (a) zinaweza kutumika na PDC kwa madhumuni yaliyobainishwa katika Mkataba huu; na (b) zinaweza kushirikiwa na PDC pamoja na wateja wake (vilevile wateja hawa wanaweza kushiriki taarifa hizi na wateja wao) kwa matumizi yao ya maudhui hayo (ikijumuisha kuchapisha Maudhui hayo ya Mtumiaji kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa mengine ya umma). Kukubaliana na Mkataba huu huashiria kwamba Mtumiaji ameridhia matumizi ya taarifa binafsi za Mtumiaji kama ilivyotarajiwa katika aya hii.

MAONI 

Mtumiaji anaipatia PDC haki isiyo ya kipekee, duniani kote, inayodumu, isiyo badilishika, bila malipo na ya kuhamishika ya kutumia kikamilifu na kuwapa leseni wengine, kwa madhumuni yoyote, mapendekezo, mawazo, maombi ya maboresho, maoni au taarifa zozote zitakazotolewa na wewe au mtu mwingine kuhusu Huduma, ikijumuisha haki zote za uvumbuzi (zote kwa pamoja, “Maoni”). Iwapo Mtumiaji ataamua kuipa PDC Maoni, PDC inaweza kuyafanyia kazi Maoni hayo bila kuwajibika au kutoa stahiki. Maoni yoyote yaliyotolewa yatachukuliwa kuwa si ya siri, na PDC itakuwa huru kutumia taarifa hizo kwa misingi isiyo kuwa na kikomo. Mtumiaji anaachilia haki zozote za kimaadili au haki za kutangazwa katika Maoni, ikiwa yapo, na haki yoyote ya kutambuliwa ambayo Mtumiaji anaweza kuwa nayo.

Unawakilisha kwamba Maoni yoyote unayotupatia hayakiuki haki za wahusika wengine, ikiwa ni pamoja na haki za hakimiliki, alama ya biashara, faragha au haki zinginezo.

AKILI BANDIA NA UCHANGANUZI WA DATA

Kama ilivyoelezewa katika Sera yetu ya Faragha, PDC inaweza kuchanganua data inayoikusanya na/au inayopokea kutoka kwa Mtumiaji, ikiwa ni pamoja na picha, video, rekodi mbalimbali na picha za skrini kwa kutumia akili bandia, na wateja wa PDC (pamoja na wateja wao) vilevile wanaweza kutumia akili bandia kwenye uchanganuzi wao wa data walioipata kutoka PDC.

SHIDA ZINAZOWEZA KUMPATA MTUMIAJI, USALAMA NA KUEPUKA HATARI

PDC inaweza, kwa busara zake binafsi, kumsaidia Mtumiaji ikiwa Mtumiaji amepatwa na shida wakati wa ukamilishaji wa Kazi. Kwa mfano, usaidizi wakati wa shida unaweza kuhusisha kumpatia kifaa kipya, kumfidia vifaa vilivyopotea au vilivyoharibiwa, au fidia ya kuumia kwa mwili, uharibifu wa mali binafsi, kupoteza saa za kazi, au faini au adhabu. Ili uombe usaidizi huo, tafadhali wasiliana na PDC kupitia: [email protected].

Usalama na utii wa sheria ni vipaumbele hapa PDC. Watumiaji wakati wote wanapaswa kuwa na mwenendo unaojali usalama wa Mtumiaji mwenyewe pamoja na wengine, na ambao haumuweki Mtumiaji au mtu yeyote mwingine katika hali itakayopelekea madhara ya kimwili au kuharibika kwa mali ya aina yoyote. PDC kwa njia yoyote ile haiungi mkono matendo yanayoweza kusababisha hatari ya kuumia mwili, kuingilia faragha au uharibifu wa mali. Watumiaji wanapaswa muda wote kutii sheria, ikiwa ni pamoja na kuwa na bima iliyo hai, kutokuingia mahali popote bila ruhusa, kutokujihusisha na matendo yaliyo kinyume cha sheria au kufanya jambo lolote lisilo salama au litakalo muweka Mtumiaji na wengine katika hatari ya aina yoyote, ikijumuisha, wakati wa kuendesha Chombo cha Usafiri. Mtumiaji hataendesha Chombo cha Usafiri bila kuweka umakini wake wote barabarani, na hataendesha Chombo cha Usafiri wakati akitumia simu au kifaa kingine cha kielektroniki.   

VIZUIZI

Mtumiaji hatatumia Huduma au Maudhui yoyote kwa kusudi lolote ambalo ni kinyume cha sheria au limepigwa marufuku na Mkataba huu, au ambalo linakiuka haki za PDC au wengine.

Mtumiaji pia anakubali kutokufanya yafuatayo:  

    • Kufikia, kubadilisha au kutumia maeneo yasiyo ya umma ya Huduma au mifumo ya kompyuta ya PDC;
    • Kujaribu kuthibitisha, kuchanganua au kujaribu kutumia udhaifu katika mfumo au mtandao wa PDC au kukiuka hatua zozote za kiusalama au uthibitishaji;
    • Kujaribu kukwepa hatua zozote za kiteknolojia zinazotekelezwa na PDC ili kulinda Huduma au Maudhui yoyote;
    • Kujaribu kutenganisha, kuchangua au kuunda upya maunzi laini yoyote inayotumiwa na Huduma;
    • Kukiuka sheria au kanuni zozote zinazotumika za kitaifa, jimbo, nchi au kimataifa;
    • Kuingilia faragha ya mtu;
    • Kuingia mahali popote pasipo pa umma au mahali ambapo watu binafsi wana matarajio ya kutosha ya faragha; au
    • Kuhimiza au kusaidia mhusika mwingine kufanya lolote kati ya vitu vilivyoorodheshwa hapo juu.

USAJILI NA ULINZI

Kama hitaji la kukagua au kukamilisha Kazi yoyote, Mtumiaji anapaswa kupakua Aplikesheni, kutengeneza akaunti, kujaza mwaka wa kuzaliwa na kuruhusu ufikiaji wa baadhi ya vipengele vya simu janja, ikiwa ni pamoja na huduma za mahali. Kulingana na mahali Mtumiaji alipo, Mtumiaji atahitajika (i) kutoa vitambulisho vya Google au Apple, au (ii) kujisajili na PDC na kuchagua nenosiri na jina la mtumiaji (“Kitambulisho cha Mtumiaji wa PDC”).

Kama hitaji la kutumia Jukwaa, Mtumiaji huenda akahitajika kutengeneza akaunti ikiwa ni pamoja na kutoa jina, mwaka wa kuzaliwa, anwani na taarifa za mawasiliano (simu na barua pepe), na pia kuhitajika kuchagua nenosiri na Kitambulisho cha Mtumiaji wa PDC. 

Mtumiaji ataipatia PDC maelezo ya usajili yaliyosahihi, kamili na ya hivi karibuni. Kushindwa kufanya hivyo kutakuwa ni uvunjaji wa Mkataba huu, kitendo kitakachoweza kusababisha kufutwa papo hapo kwa akaunti ya Mtumiaji.

Mtumiaji hawezi (i) kuchagua au kutumia kama Kitambulisho cha Mtumiaji wa PDC jina la mtu mwingine kwa nia ya kujifanya kuwa mtu huyo; (ii) kutumia kama Kitambulisho cha Mtumiaji wa PDC jina lililo na haki za mtu yeyote isipokuwa Mtumiaji bila idhini sahihi: au (iii) kutumia kitambulisho cha mtu mwingine au kwa njia yoyote ile kujifanya kuwa yeye ni mtu mwingine. PDC ina haki ya kukataa usajili, au kughairisha Kitambulisho cha Mtumiaji wa PDC au usajili mwingine kwa busara yake binafsi.

Mtumiaji atakuwa na jukumu la kulinda usiri wa nenosiri lake kama mtumiaji wa PDC na taarifa nyingine za akaunti.

Mtumiaji yeyote anayejisajili na PDC kutoka nje ya Marekani anakubali kutotumia Aplikesheni au kupata Huduma akiwa ndani ya Marekani.

FIDIA

Mtumiaji anawajibika kwa shughuli zote za Mtumiaji zinazohusiana na Huduma, ikiwa ni pamoja na kuumia kwa mwili, kuharibika kwa mali au upotevu wowote mwingine unaotokana na Mtumiaji unaohusiana na Kazi. Kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria, Mtumiaji ataitetea, kuifidia, na kuiacha bila lawama PDC, washirika wake pamoja na wafanyakazi, makontrakta, wakurugenzi, wasambazaji na wawakilishi wa PDC na washirika wake dhidi ya dhima, madai na gharama zote, pamoja na gharama zinazofaa za mawakili, ambazo hazikusababishwa na uzembe au mwenendo mbaya wa PDC na zinazotokana na Mtumiaji (i) kutumia au kutumia vibaya Huduma; (ii) kufikia sehemu yoyote ya Huduma, au (iii) kukiuka Mkataba huu.  

KANUSHO LA DHIMA

ISIPOKUWA KAMA INATAKIWA VINGINEVYO KISHERIA, HUDUMA HII (PAMOJA, LAKINI SI TU, APLIKESHENI, TOVUTI NA MAUNZI TEPE YOYOTE) INAWASILISHWA “KAMA ILIVYO”, BILA DHAMANA YA AINA YOYOTE, AIDHA YA MOJA KWA MOJA AU KWA KUTHIBITISHWA, IKIWA PAMOJA NA, KUTOKUWA NA KIKOMO, DHAMANA YA UUZAJI, UFAAFU KWA MATUMIZI FULANI AU UKOSEFU WA UKIUKAJI. PDC HAITOI DHAMANA YOYOTE  KUWA (I) HUDUMA HAINA VIRUSI AU VIPENGELE VINGINE VYENYE MADHARA, (II) HUDUMA ITAKUWA SALAMA AU ITAPATIKANA KWA WAKATI WOTE AU MAHALI POPOTE, (III) KASORO AU MAKOSA YOYOTE YATASAHIHISHWA, AU (IV) MATOKEO YA KUTUMIA HUDUMA HIYO YATAKIDHI MAHITAJI YA MTUMIAJI, HASA, PDC HAITOI DHAMANA KUHUSU USAHIHI WA DATA YOYOTE ILIYOWASILISHWA KUPITIA HUDUMA HIYO. MATUMIZI YA MTUMIAJI YA HUDUMA YATABAKI KUWA WAJIBU WA MTUMIAJI MWENYEWE.

SHERIA KATIKA BAADHI YA MAJIMBO AU NCHI HAZIRUHUSU VIKOMO JUU YA DHAMANA INAYODOKEZWA AU KUTOJUMUISHWA AU KIKOMO CHA UHARIBIFU FULANI. IKIWA SHERIA HIZI ZINAKUHUSU, BAADHI AU KANUSHO LOTE HAPO JUU, KUTOJUMUISHWA AU VIKOMO HAVITAKUHUSU, NA UNAWEZA KUWA NA HAKI ZA ZIADA. 

KIKOMO CHA DHIMA

HAKUNA TUKIO AMBALO PDC, MAAFISA, WAKURUGENZI, WAMILIKI, WAFANYAKAZI, MAWAKALA, WASHIRIKA AU WASAMBAZAJI WAKE WATAWAJIBISHWA CHINI YA MKATABA, SHERIA YA TORT, DHIMA, UWAJIBIKAJI MKAKATI, UZEMBE AU NADHARIA YOYOTE YA KISHERIA INAYOHUSISHA HUDUMA ZOZOTE (AU DATA AU TAARIFA NYINGINE INAYOPATIKANA KUPITIA HUDUMA): (I) KWA FAIDA YOYOTE ILIYOPOTEA AU MADHARA YA KIPEKEE, YASIYO YA MOJA KWA MOJA, AU ADHABU ZA FIDIA ZA AINA YOYOTE ILE, HATA KAMA YANAWEZA KUTABIRIKA, (II) KWA HITILAFU ZOZOTE, VIRUSI, FARASI ZA TROJAN, AU NYINGINEZO (BILA KUJALI CHANZO CHA ASILI), (III) KWA MAKOSA AU KUTOKUJUMUISHWA KWA DATA AU TAARIFA ZOZOTE AU KWA HASARA AU UHARIBIFU WA AINA YOYOTE UNAOTOKANA  NA MATUMIZI YA DATA AU TAARIFA YOYOTE ILIYOCHAPISHWA, KUTUMWA KWA BARUA PEPE, KUSAMBAZWA AU KUFANYWA IPATIKANE KUPITIA HUDUMA, AU (IV) KWA UHARIBIFU WOWOTE WA MOJA KWA MOJA UNAOZIDI (KWA UJUMLA) $100.00 (USD) (IKIWA MTUMIAJI AMELIPIA HUDUMA AU KIPENGELE, NA MALIPO HAYO NI ZAIDI YA $100.00. ) KIFUNGO CHA DHIMA KITAONGEZWA HADI KUFIKIA KIASI HICHO).  Aidha, PDC haitahukumiwa kwa hasara yoyote au dhima inayosababishwa, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja, kutokana na Mtumiaji kushindwa kufikia au kwa vyovyote vile kutokutumia Huduma (ikiwa ni pamoja na, lakini si tu, ucheleweshaji wowote au kukatishwa kutokana na hitilafu za vifaa vya kielektroniki au mitambo, mashambulizi ya huduma, hali inayosababisha kushindwa kuchakata takwimu, matatizo ya mawasiliano ya simu au mtandao au hitilafu za huduma muhimu.)

SHERIA KATIKA BAADHI YA MAJIMBO AU NCHI HAZIRUHUSU KUTOKUJUMUISHA AU UWEKAJI WA KIKOMO KWENYE FIDIA ZINAZOTOLEWA MAHAKAMANI KUTOKANA NA UVUNJIFU WA MOJA KWA MOJA AU USIYO WA MOJA KWA MOJA WA MKATABA, HIVYO VIKOMO NA HALI ZA KUTOKUJUMUISHWA ZILIZO HAPO JUU HUENDA ZISIKUHUSU. KWA AJILI YA KUONDOA SHAKA, VIKOMO NA HALI ZA KUTOKUJUMUISHWA ZILIZO KATIKA AYA ILIYOTANGULIA HAZIWAHUSU WAKAZI WA NEW JERSEY. 

UKOMESHAJI

PDC inaweza kusitisha uwezo wa Mtumiaji kufikia baadhi au Huduma nzima wakati wowote, bila kuwepo kwa sababu, itakayofanya kazi baada ya kusitishwa kwa akaunti yako (ikiwa PDC itagundua kuwa kuna tishio la papo hapo kwa PDC, inaweza kusitisha upatikanaji huo bila notisi). 

Mtumiaji anaweza kusitisha akaunti ya Mtumiaji na usajili wake na PDC wakati wowote kwa kufuta Aplikesheni kutoka kwenye kifaa cha Mtumiaji, kuacha kutumia Huduma na anaweza kuwasiliana na PDC kupitia: [email protected] akiwa na maswali yoyote. 

Baada ya kusitishwa, Mtumiaji hatafikia tena (au kujaribu kufikia) Huduma.

Masharti yote ya Mkataba huu ambayo kwa asili yake yanapaswa kuendelea kudumu hata baada ya kusitishwa kwake, yataendelea kudumu hata baada ya kusitishwa, ikijumuisha, bila kizuizi, utatuzi wa migogoro, mamlaka ya kisheria na uchaguzi wa sheria (pamoja na hati ya kuachilia haki ya dai binafsi la mahakamani au la kikundi), masharti ya umiliki wa Maudhui, kanusho za dhima na kikomo cha dhima.

UTATUZI WA MIGOGORO, MAMLAKA YA KISHERIA NA UCHAGUZI WA SHERIA

Mkataba huu utatawalwa na kuundwa kulingana na sheria za jimbo la California, na itakuwa kama Mkataba huu umeundwa ndani ya California  kati ya wenyeji wawili wa California.

Pande zote mbili zinakubaliana na mamlaka binafsi ya kisheria huko San Francisco, California, Marekani. Kwa masuala yoyote ambayo hayako chini ya usuluhishi, au kulazimisha usuluhishi au kudhibitisha, kurekebisha, kuacha au kutoa hukumu juu ya uamuzi wa msuluhishi, wahusika wanakubali mamlaka binafsi na ukumbi katika mahakama za jimbo na shirikisho zilizopo San Francisco, California, Marekani au kitengo kingine chochote cha Wilaya ya Kaskazini ya California ikiwa kesi itapangwa na mahakama ya serikali ya shirikisho kuendeshwa na kitengo kilichopo kwenye Wilaya ya Kaskazini tofauti na Kitengo cha San Francisco cha Wilaya ya Kaskazini ya California.

Isipokuwa kama ilivyoelezwa hapa, mzozo wowote, madai au utata unaotokana au unaohusiana kwa njia yoyote na Mkataba huu, Aplikesheni, Tovuti, Jukwaa au Huduma, au utangazaji wake, ikijumuisha uamuzi wa mawanda au utumiaji wa makubaliano haya kwa usuluhishi na madai ambayo yalipatikana kabla ya kuingia Mkataba huu, yatatatuliwa kwa usuluhishi kwa mujibu wa sheria na taratibu za JAMS, Inc. (“JAMS”) zinazotumika wakati usuluhishi unapoanzishwa. Madai pekee ambayo hayajajumuishwa katika usuluhishi ni madai yanayohusu ukiukaji, ulinzi au uhalali wa siri za biashara, hakimiliki, alama ya biashara au haki za hataza za watoa leseni wako, PDC au wa PDC.

Makubaliano haya ya usuluhishi yatadumu hata baada ya kusitishwa kwa Mkataba huu. Usuluhishi utakuwa mbele ya msuluhishi mmoja. Katika usuluhishi wowote unaotokana au unaohusiana na Mkataba huu, msuluhishi hawezi kutoa uamizi wa utoaji wa fidia yoyote kinyume cha masharti ya Mkataba huu. Msuluhishi atachaguliwa kwa makubaliano ya pamoja ya wahusika. Endapo wahusika hawataweza kukubaliana juu ya msuluhishi ndani ya siku thelathini (30) baada ya mhusika aliyeanzisha kumpatia mhusika mwingine notisi ya maandishi kwamba anapanga kutafuta usuluhishi, JAMS itafanya uteuzi wa msuluhishi kwa mujibu wa sheria zake. Uamuzi wa maandishi wa msuluhishi utakuwa ndiyo wa mwisho na unaowafunga wahusika na kutekelezwa katika mahakama yoyote. Mchakato wa usuluhishi utaanzishwa na utafanyika San Francisco, California, kwa kutumia lugha ya Kiingereza, isipokuwa kama itakubaliwa vinginevyo na wahusika, na inaweza kufanywa kwa njia ya mtandao. Usuluhishi wowote chini ya Mkataba huu utafanyika kwa misingi ya mtu binafsi: usuluhishi wa kikundi na madai ya mahakamani ya kikundi hayaruhusiwi. UNAELEWA NA KUKUBALI KWAMBA KWA KUINGIA KWENYE MKATABA HUU, WEWE NA PDC KWA PAMOJA MNAACHILIA HAKI YENU YA KUFUNGUA KESI MAHAKAMANI YENYE WAAMUZI AU KUSHIRIKI KESI YA KIKUNDI. 

ANUWAI

Kushindwa kwa mhusika yeyote kutumia kwa njia yoyote ile haki yake yoyote iliyoelezwa katika Mkataba huu haitachukuliwa kuwa ni kuondolewa kwa haki yoyote zaidi hapa chini. 

Unakubali kwamba wewe si mfanyakazi, wakala, mshirika au mbia wa PDC, na hauna mamlaka ya aina yoyote ya kuifunga PDC kwa namna yoyote ile.

PDC haitawajibika kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa mkataba huu ambapo kushindwa huko kunatokana na sababu yoyote inayoeleweka na iliyo nje ya uwezo wa PDC, ikijumuisha, bila kikomo, kuharibika au hitilafu kwenye mitambo ya kielektroniki au mawasiliano (pamoja na kuingiliwa kwa “kelele za laini”).

Endapo kifungu chochote cha Mkataba huu kitapatikana kuwa hakitekelezeki au ni batili, kifungu hicho kitawekewa kikomo au kuondolewa kwa kiwango cha chini kinachohitajika ili Mkataba huu uendelee kuweza kutumika, kutekelezeka pamoja na kuwa na nguvu kamili.

Mkataba huu hauwezi kukabidhiwa, kuhamishwa au Mtumiaji kumpatia leseni mwingine isipokuwa kwa idhini iliyoandikwa awali na PDC. PDC inaweza kuhamisha, kukabidhi Mkataba huu na wajibu pamoja na haki zilizopo ndani yake bila idhini.

Isipokuwa ikiwa imeelezwa vinginevyo hapa, pande zote mbili zinakubali kwamba Mkataba huu (kama ulivyojaliziwa na masharti yoyote mahususi ya Kazi ambayo Mtumiaji atafanya, sheria yoyote ya PDC, taratibu au sera, ikiwa ni pamoja na, Sera ya Faragha iliyojumuishwa ndani ya mkataba huu, zinazotumika wakati wa kipindi cha Mkataba huu, na sera na sheria za jukwaa la app ambayo Mtumiaji aliipata Aplikesheni) ni makubaliano kamili ya wahusika. Ikiwa kuna mgongano kati ya Mkataba huu na makubaliano au sera za awali, basi masharti ya Mkataba huu ndio yatatumika. Marekebisho yote lazima yawe katika maandishi yaliyotiwa saini na pande zote mbili, isipokuwa kama imeandikwa vinginevyo humu ndani.

Mtumiaji atatii sheria zote zinazotumika za shirikisho, jimbo na eneo husika, ikijumuisha sheria za kodi ya mapato.

Mkataba huu ni batili pale unapopingwa kisheria, na haki ya kufikia Huduma inabatilishwa katika maeneo hayo.