Sera ya Faragha ya Premise

Tarehe ya Kuanza Kutumika: Tarehe 1 Aprili, 2024

Kama Premise Data Corporation (“Premise”) tunafahamu unajali jinsi taarifa zako binafsi zinavyotumiwa na kushirikiwa na tunalichukulia suala la faragha yako kwa uzito mkubwa. Tafadhali soma yafuatayo ili upate maelezo zaidi kuhusu taarifa binafsi zinazokusanywa, kutumiwa na kushirikiwa nasi. Maneno yoyote yenye herufi kubwa tunayotumia kwenye Sera hii ya Faragha bila kufafanua, yamefafanuliwa katika Masharti ya Huduma: https://tos.premise.com/terms-of-use/.

Kwa kutumia au kufikia Huduma, ikijumuisha kutumia tovuti, malango au majukwaa yetu kwa namna yoyote ile au kupakua aplikesheni zetu za vifaa vya mkononi, kukagua au kukamilisha Kazi (kama ilivyoelezwa kwenye Masharti ya Huduma) na kujiunga na Pochi ya Premise, unakubali taratibu na sera zilizoelezewa kwenye Sera hii ya Faragha na unaridhia ukusanyaji, matumizi na ushiriki wetu wa taarifa zako binafsi kwa njia zilizoorodheshwa hapo chini.

Elewa Nafasi yako Kwetu

Premise kwenye sera hii inatumia maneno kama “Mteja”, “Mchangiaji” na “Mgeni” ili kueleza nafasi mbalimbali za uhusiano baina ya Premise, huduma zake na mazingira. Nafasi hizi zinafasiliwa kama ifuatavyo:

    • Mteja: Ikiwa wewe ni mtu unayetekeleza Makubaliano Makuu ya Huduma au makubaliano mengine ya mteja kupitia sisi (“Makubaliano ya Mteja”) (au ni mwajiriwa/mshauri wa kampuni iliyotekeleza Makubaliano ya Mteja na unafikia Huduma kupitia sisi kama mwajiriwa/mshauri wa kampuni hiyo), au umeidhinishwa na Premise kwa njia dhahiri kufikia mojawapo kati ya majukwaa au malango mahususi kwa ajili ya wateja, utajulikana kama Mteja kwenye Sera hii ya Faragha.
    • Mchangiaji: Ikiwa utapakua aplikesheni zetu za vifaa vya mkononi, utajulikana kama Mchangiaji kwenye Sera hii ya Faragha.
    • Mgeni: Watu wengine wote watajulikana kama Wageni.

Masharti yaliyomo kwenye Sehemu ya Kwanza ya Sera hii ya Faragha yatatumika kwa Wateja, Wachangiaji na Wageni.  Masharti yaliyomo kwenye Sehemu ya Pili yatatumika ikiwa wewe ni Mteja. Masharti yaliyomo kwenye Sehemu ya Tatu yatatumika ikiwa wewe ni Mchangiaji. Masharti yaliyomo kwenye Sehemu ya Nne yatatumika kwa Wachangiaji, Wateja na Wageni ambao ni wakazi wa California au majimbo mengineyo yenye haki zinazofanana.

 

SEHEMU YA KWANZA – MASHARTI KWA AJILI YA KILA MTU – WATEJA, WACHANGIAJI NA WAGENI

Sera hii ya Faragha inatumika kwenye aplikesheni, tovuti, majukwaa na bidhaa pamoja na huduma za Premise zinazopatikana kwenye au katika aplikesheni, tovuti au malango mengine ya mtandaoni. Premise hukusanya taarifa kukuhusu unaposakinisha aplikesheni yetu ya kifaa cha mkononi na kupitia shughuli na mawasiliano mengine kati yako na sisi kupitia huduma zetu za mtandaoni (ikiwa ni pamoja na tovuti, malango na majukwaa yetu) au vinginevyo. Kumbuka kwamba matumizi yako ya Huduma hii wakati wote hutawalwa na Masharti ya Huduma, yanayoshirikisha Sera hii ya Faragha. Huduma inamilikiwa na kuendeshwa na Premise, na Sera hii ya Faragha inatumika katika taarifa zilizokusanywa na kutumiwa na Premise.

Tunaweza kuhamisha taarifa zilizoelezewa kwenye Sera hii ya Faragha, kuzichakata na kuzihifadhi nchini Marekani, ambapo huenda kuna kiwango kidogo zaidi cha sheria za ulinzi wa data ikilinganishwa na nchi unayoishi. Endapo tutafanya hivyo, tutachukua hatua stahiki kulinda taarifa zako binafsi kulingana na Sera hii ya Faragha pamoja na sheria zinazotumika.

Tunaendelea kujitahidi kuboresha Huduma zetu. Pia, tunaweza kubadilisha Sera hii ya Faragha mara kwa mara. Tutakuarifu kuhusu mabadiliko kupitia ujumbe wa ndani ya aplikesheni, kuchapisha notisi katika mitandao ya kijamii stahiki, kuchapisha Sera ya Faragha iliyosasishwa kwenye tovuti yetu, majukwaa na/au kwa kutumia namna nyinginezo. Tafadhali kumbuka kwamba, ikiwa ulichagua kutokupokea barua pepe za notisi za kisheria kutoka kwetu (au hujatupatia anwani yako ya barua pepe), notisi hiyo ya kisheria bado itatawala matumizi yako ya Huduma na bado unawajibika kuzisoma na kuzielewa. Endapo utatumia Huduma baada ya mabadiliko yoyote kwenye Sera ya Faragha kuchapishwa, utumiaji huo utaonyesha kukubaliana na mabadiliko yote. Matumizi ya taarifa tunazokusanya yatatawalwa na Sera ya Faragha itakayotumika wakati taarifa hizo zinakusanywa.

MAWANDA NA MATUMIZI

Sera hii ya Faragha inatumika kwa watu wote popote duniani wanaofikia na kutumia Huduma zozote.

Hatukusanyi wala kuomba, kwa kufahamu, taarifa binafsi kutoka kwa yeyote aliye chini ya umri wa miaka 18 au umri wa kuwa mtu mzima katika nchi ambayo anaishi au alipo wakati akitumia Huduma, umri wowote uliyo mdogo zaidi (kwa jumla, “Kima cha Chini cha Umri”). Tafadhali usijaribu kutumia Huduma au kututumia taarifa zozote binafsi ikiwa una umri chini ya Kima cha Chini cha Umri, vilevile tafadhali usitutumie taarifa binafsi za yeyote aliye chini ya Kima cha Chini cha Umri au aliye chini ya miaka 13, umri wowote uliyo mdogo zaidi. Iwapo tutagundua kwamba tumekusanya taarifa binafsi kutoka kwa mtu aliye chini ya Kima cha Chini cha Umri au aliye chini ya miaka 13, umri wowote uliyo mdogo zaidi,  tutafuta taarifa hizo haraka iwezekanavyo. Ikiwa unaamini mtu aliye chini ya Kima cha Chini cha Umri ametupatia taarifa binafsi au sisi tumetoa taarifa binafsi za mtu aliye chini ya Kima cha Chini cha Umri au aliye chini ya miaka 13, umri wowote uliyo mdogo zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia: [email protected].

UKUSANYAJI NA MATUMIZI YA TAARIFA

Taarifa Tunazokusanya Kupitia Matumizi yako ya Huduma

Tunakusanya taarifa zinazohusu jinsi unavyotumia Huduma, mapendeleo uliyoonyesha na mipangilio uliyochagua. Katika baadhi ya hali, tunakusanya taarifa hizi kupitia matumizi ya vidakuzi, vitambulisho vya pikseli na teknolojia nyinginezo zinazofanana ambazo huunda na kudumisha vitambulishi vya kipekee. Kupitia vidakuzi tunavyoweka kwenye kivinjari au kifaa chako, pia tunaweza kukusanya taarifa kuhusu shughuli zako za mtandaoni baada ya wewe kuondoka kwenye Huduma. Taarifa hii hutuwezesha kuboresha Huduma na kufanya hali ya matumizi mtandaoni kuwa mahususi kwako, na vinginevyo kama ilivyoelezwa kwenye Sera hii ya Faragha. 

Vilevile, tunakusanya taarifa unazotupatia kwa njia ya moja kwa moja pamoja na taarifa unazotupatia kupitia matumizi ya akaunti za wahusika wengine.

Kivinjari chako kinaweza kukupatia chaguo la “Do Not Track/Usifuatilie”, ambalo linakuwezesha uashirie kwa waendesha tovuti, aplikesheni na huduma za mtandaoni (ikiwa ni pamoja na huduma za matangazo yanayotokana na mambo unayofuatilia mtandaoni) kwamba hutaki watoa huduma hao wafuatilie baadhi ya shughuli zako za mtandaoni kadri muda unavyosonga na kwenye tovuti mbalimbali. Kwa wakati huu, Huduma haitumii chaguo la “Do Not Track/Usifuatilie”, ikimaanisha kwamba tunakusanya taarifa kuhusu shughuli zako za mtandaoni wakati unatumia Huduma na baada ya kuondoka katika Huduma. Kwa kutumia Huduma yetu, unaridhia kwa njia dhahiri ukusanyaji huu wa taarifa.

Google, Bing na matangazo ya mitandao ya kijamii pamoja na makampuni mengine yanayofanana na haya ambayo Premise hufanya nayo kazi, huenda yakakusanya au kupokea taarifa zako zinazokutambulisha binafsi, zinazohusu shughuli zako mtandaoni kadri muda unavyosonga na katika tovuti mbalimbali kutoka kwenye Huduma na aplikesheni nyinginezo, na kutumia taarifa hizo ili kutoa huduma ya kufanya vipimo na kukuonyesha matangazo. Kwa kutumia Huduma, unaridhia ukusanyaji na matumizi ya taarifa kwa ajili ya kufanya matangazo yawe mahususi kwako. Unaweza kujiondoa kwenye Google Analytics kwa kutumia nyongeza ya kivinjari ifuatayo: https://tools.google.com/dlpage/gaoptout/.

Tunatumia uchanganuzi ili kutusaidia kuchanganua jinsi watumiaji wetu wanavyotumia Huduma. Google Analytics hutumia vidakuzi kukusanya taarifa kama vile, mara ngapi watumiaji wetu wanatembelea Huduma, ni kurasa zipi wanatembelea na ni tovuti zipi walitembelea kabla ya kuja kwenye Huduma. Tunaweza kutumia taarifa tunazopokea kutoka Google Analytics ili kuboresha Huduma yetu au kukutumia ujumbe wa matangazo unaohusu Huduma yetu. Google Analytics hukusanya anwani ya IP uliyokabidhiwa siku unayotembelea Huduma, lakini haikusanyi jina lako wala maelezo mengine yanayokutambulisha binafsi. Hatuchanganyi taarifa zinazozalishwa kupitia matumizi ya Google Analytics na taarifa yoyote ya kukutambua binafsi. Ingawaje, Google Analytics inaweka Kidakuzi kinachosalia ili kukutambua kama mtumiaji wa kipekee wakati mwingine unapotembelea Huduma, Kidakuzi hiki hakiwezi kutumika na yoyote mwigine isipokuwa Google. Uwezo wa Google wa kutumia na kushiriki taarifa zilizokusanywa na Google Analytics kuhusu ziara zako kwenye Huduma zinatawalwa na Sheria na Masharti ya Google Analytics na Sera ya Faragha ya Google. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu Google Analytics katika: http://www.google.com/policies/privacy/partners/.

Tunapohitajika chini ya sheria zinazotumika kuomba ridhaa yako ili kutumia vidakuzi visivyo vya lazima, tunaomba ridhaa hiyo kupitia nyenzo yetu ya udhibiti wa vidakuzi.

Taarifa za Ziada

Tafadhali soma sehemu zilizopo hapo chini kwenye Sera hii ya Faragha zinazohusiana na wewe kwa ufafanuzi wa taarifa za ziada tunazokusanya.

KUBAKI NA TAARIFA

Tutabaki tu na taarifa zako binafsi kwa kipindi kinachofaa ili kutimiza madhumuni yaliyotufanya tukusanye taarifa hizo, ikiwa ni pamoja na kutimiza mahitaji ya kisheria, kikodi, kiudhibiti, kiuhasibu au ya kuandaa ripoti. Tunaweza kubaki na taarifa zako binafsi kwa kipindi kirefu zaidi ikiwa kuna lalamiko au sababu zinazotufanya tuamini kwamba kuna uwezekano wa kufunguliwa kesi ya madai kutokana na uhusiano wetu na wewe. Ili kuamua kipindi sahihi cha kubaki na taarifa zako binafsi, tunaangalia idadi, asili na unyeti wa taarifa zako binafsi, athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi au ufichuzi usiyoidhinishwa wa taarifa zako binafsi, madhumuni ya kuchakata taarifa zako binafsi na kama tunaweza kufikia madhumuni hayo kupitia njia nyinginezo, na mahitaji ya kisheria, kikodi, kiudhibiti na mengine yanayohusika.

ULINZI WA DATA KATIKA NCHI ZA UMOJA WA ULAYA

Sehemu hii inatumika katika ukusanyaji, upokeaji au uchakataji mwingine wa taarifa binafsi za watu wanaoishi kwenye Eneo la Kiuchumi la Ulaya (“EEA”) na/au Uingereza (“UK”), unaofanywa nasi au kwa niaba yetu.

Tutafanya jitihada za kuchakata taarifa zako binafsi kwa mujibu wa sheria za faragha zinazotumika, ikijumuisha bila ukomo, pale itakapofaa, Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data (Sheria (EU) 2016/679) (“EU GDPR”), EU GDPR kwa kuwa inaunda sehemu ya sheria ya Uingereza na Welisi, Skotilandi na Ayalandi ya Kaskazini kutokana na kifungu cha 3 cha Sheria ya Kujiondoa Umoja wa Ulaya ya 2018 (“UK GDPR”), Sheria ya UK ya Ulinzi wa Data ya 2018 na Kanuni za Faragha na Mawasiliano ya Elektroniki (Maelekezo ya EC) ya 2003 (“Sheria za Ulaya za Faragha ya Data”). 

Maelezo ya kina juu ya aina ya taarifa binafsi tunazozichakata, misingi ya kisheria ya uchakataji huo na namna tunavyoweza kushiriki taarifa zako binafsi yanatolewa hapo chini.

Chini ya Sheria za Ulaya za Faragha ya Data zinazotumika, wewe binafsi unaweza kutumia haki zifuatazo:

    • Kuomba kufikia taarifa zako binafsi.
    • Kuomba kusahihishwa kwa taarifa binafsi tulizonazo kukuhusu.
    • Kuomba kufutwa kwa taarifa zako binafsi.
    • Kupinga uchakataji wa taarifa zako binafsi.
    • Kuomba kizuizi dhidi ya uchakataji wa taarifa zako binafsi.
    • Kuomba kuhamishwa kwa taarifa zako binafsi kuja kwako au kwa muhusika mwingine.
    • Muda wowote kuondoa ridhaa pale tunapohitaji ridhaa ya kuchakata taarifa zako binafsi.

Ili utekeleze mojawapo kati ya haki hizi, tafadhali wasiliana nasi kama ilivyoonyeshwa hapa chini. Tutafanya jitihada za kukupatia majibu ndani ya kipindi cha mwezi mmoja wa kupokea ombi lako, isipokuwa kama ombi litakuwa na ugumu katika utekelezaji wake, ambapo inaweza kuchukua muda mrefu zaidi. Pia, tunaweza kuomba taarifa fulani kutoka kwako zitakazotusaidia kuthibitisha utambulisho wako pamoja na haki yako ya kufikia taarifa binafsi hizo (au utekelezaji wa haki zozote zilizoainishwa hapo juu). Tafadhali fahamu ya kwamba baadhi ya haki hizi zinaruhusa ya kutokufanya jambo au kutokufuata kanuni, ambazo tutazitumia kulingana na Sheria za Ulaya za Faragha ya Data zitakazotumika. Hususani, ikiwa ulitupatia ridhaa ya kuchakata na baadaye ukaondoa ridhaa hiyo, tunaweza kuchakata taarifa hiyo binafsi ikiwa tunasababu nyingine ya kisheria ya kufanya hivyo.

Tunaweza kuhamisha taarifa binafsi tunazochakata ndani ya EEA au UK kwenda nje ya EEA au UK, ikijumuisha kwenda nchini Marekani. Taarifa zako binafsi zitahamishwa tu kwenda nje ya EEA au UK inapohitajika na kwa mujibu wa Sheria za Ulaya za Faragha ya Data zinazotumika, ambazo zinaweza kujumuisha kuchukua hatua za ziada za kimkataba au hatua nyinginezo zilizopitishwa na kukubaliwa na Ofisi ya Kamishna wa Taarifa wa UK au Kamisheni ya Ulaya au mamlaka yoyote nyingine ya EEA yenye haki hiyo ya kisheria.

WASILIANA NASI

Ikiwa una maswali yoyote yanayohusu Sera hii ya Faragha, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwenda: [email protected], au tuandikie barua kwenda: Premise Data Corporation, Inc., Attn: Legal, 405 W 13th Street, 3rd Floor, New York, NY 10014, United States of America au kupitia mojawapo kati ya anwani za wawakilishi wetu wa ulinzi wa data zilizopo hapo chini.

umechagua wawakilishi wafuatao wa ulinzi wa data nchini UK na EEA ambao, pamoja na majukumu mengineyo, wanaweza kupokea kwa niaba yetu mawasiliano yoyote kutoka kwako au mamlaka yoyote ya usimamizi yenye haki hiyo kisheria:

    1. Uingereza:
      Adam Brogden [email protected]
      Tel +44 1772 217800
      1st Floor Front Suite
      27-29 North Street, Brighton
      England
      BN1 1EB
    2. Eneo la Kiuchumi la Ulaya
      Adam Brogden [email protected]
      Tel +35315549700
      INSTANT EU GDPR REPRESENTATIVE LTD
      Office 2,
      12A Lower Main Street, Lucan Co. Dublin
      K78 X5P8
      Ireland

Endapo utaamini hatujatatu wasiwasi wako au vinginevyo utaamua kufanya hivyo, una haki chini ya Sheria za Ulaya za Faragha ya Data kutuma lalamiko kwenda kwenye mamlaka ya ulinzi wa data yenye haki ya kisheria nchini UK au EEA, pale inapofaa. Ikiwa upo nchini UK, mawasiliano ya Ofisi ya Kamishna wa Taarifa wa UK yanapatikana kwenye tovuti ya: www.ico.org.uk.

SEHEMU YA PILI – MASHARTI YA ZIADA KWA WATEJA

Pamoja na masharti yaliyomo kwenye Sehemu ya Kwanza hapo juu, masharti yaliyomo kwenye Sehemu ya Pili pia yatatumika kwa Wateja wetu.

Ikitokea mkanganyiko kati ya Makubaliano ya Mteja yanayotumika kwako na Sera hii ya Faragha, basi masharti yaliyomo kwenye Makubaliano hayo ya Mteja ndiyo yatatawala kwa kiwango kinachoruhusiwa kisheria na katika kipindi ambacho Makubaliano hayo ya Mteja yatatumika.

UKUSANYAJI NA MATUMIZI YA TAARIFA

Aplikesheni za kivinjari za Premise kwa ajili ya Wateja hukusanya data na metadata zinazohusiana na kuingia kwenye akaunti, uthibitishaji na taarifa za akaunti. Sentry, Amplitude na FullStory na makampuni mengine yanayofanana na haya ambayo Premise hufanya nayo kazi, yanaweza kukusanya au kupokea taarifa zinazokutambulisha binafsi kuhusu shughuli zako mtandaoni kadri muda unavyosonga na matumizi ya aplikesheni za Premise mahususi kwa wateja. Taarifa hizi hutumiwa tu kwa madhumuni ya kuboresha aplikesheni za Premise mahususi kwa wateja na haziuzwi wala kushirikiwa na wahusika wengine.

Taarifa za mauzo, mawasiliano na ushirikiano zinakusanywa katika mifumo ya mahesabu na mawasiliano iliyokubaliwa kama vile, Salesforce, Google Workspace na Microsoft 365 pamoja na mifumo mingine iliyokubaliwa ambayo ni faragha na iliyotengwa; inayoweza kufikiwa tu na wafanyakazi wa Premise wenye idhini.

SEHEMU YA TATU – MASHARTI YA ZIADA KWA WACHANGIAJI

Pamoja na masharti yaliyomo kwenye Sehemu ya Kwanza hapo juu, masharti yaliyomo kwenye Sehemu ya Tatu yatatumika pia kwa Wachangiaji wetu.

Aplikesheni za Premise za vifaa vya mkononi ni nyenzo zinazokusanya data kuhusu dunia inayokuzunguka. Kwa kupakua mojawapo kati ya aplikesheni za Premise au kwa kujiunga na Pochi ya Premise, unaridhia ukusanyaji, ushiriki au uuzaji wa taarifa zako binafsi, ikijumuisha picha, video, rekodi mbalimbali, picha na picha za skrini, kama ilivyoelezwa kwenye Sera hii ya Faragha na unakubali kwamba Premise inaweza kuwapatia wateja wake taarifa zako pamoja na uchambuzi wa taarifa hizo kwa matumizi yao na wateja wao, ndani na nje. Tunaweza kutoa notisi za ziada kuhusu ukusanyaji na matumizi ya taarifa binafsi (ikiwa ni pamoja na picha, rekodi mbalimbali, picha, picha za skrini na rekodi za sauti) ndani ya aplikesheni au kwenye maelezo ya kazi husika.

UKUSANYAJI WA TAARIFA

Orodha ifuatayo inaonyesha baadhi ya data tunazokusanya na kwa nini tunazikusanya, na, kwa madhumuni ya Sheria za Ulaya za Faragha ya Data, misingi ya kisheria ya uchakataji. Tumetoa maelezo zaidi kuhusu taarifa binafsi tunazokusanya kwenye sehemu inayofuata ya Sera hii ya Faragha. Pale kwenye jedwali palipoainishwa msingi zaidi ya mmoja wa kisheria, unapaswa uwasiliane nasi ikiwa unahitaji maelezo zaidi kuhusu msingi mahususi wa kisheria tunaoutegemea ili kuchakata taarifa zako binafsi.

Tunachokusanya Kwa nini tunakusanya data hii Msingi wa kisheria (chini ya Sheria za Ulaya za Faragha ya Data)
Vitambulishi, m.f., jina, barua pepe, vitambulishi vya mtandaoni (kama vile, jina la mtumiaji), vitambulishi vya mtumiaji vinavyoweza kuwekwa upya vinavyotolewa na mfumo endeshi wa kifaa, manenosiri, saini za kidijitali Ili kukutambua, kufuatilia Kazi ulizokamilisha, kuwasiliana na wewe kuhusu akaunti yako, kukutumia taarifa mpya kuhusu Kazi na Huduma, kudumisha na kuendesha Huduma yetu, kufuatilia shughuli na kuboresha utoaji pamoja na kutambua shughuli, kukusanya taarifa kwa ajili ya wateja na washirika wetu na kupambana dhidi ya udanganyifu.
  • Ili kutimiza mkataba na wewe
  • Maslahi halali
  • Ni lazima ili kutii wajibu wa kisheria (kudhibiti udanganyifu)
icha, video na rekodi mbalimbali, ikijumuisha rekodi za sauti, picha na picha za skrini Ili kukutambua, kufuatilia na kuthibitisha Kazi ulizokamilisha, kufuatilia shughuli na kuboresha utoaji pamoja na kutambua shughuli, kukusanya taarifa, ikiwa ni pamoja na picha, video, rekodi mbalimbali, picha na picha za skrini, kwa ajili ya wateja na washirika wetu na kupambana dhidi ya udanganyifu. Hii inamaanisha taarifa na picha, video, rekodi mbalimbali, picha na picha za skrini unazotupatia huenda zikachapishwa na wahusika wengine (wateja wetu au wateja wao) kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa mengineyo.
  • Maslahi halali
  • Ni lazima ili kutii wajibu wa kisheria (kudhibiti udanganyifu)
  • Idhini
Mahali Kutambua watumiaji vizuri zaidi kwa ajili ya Kazi, kukusanya taarifa kwa ajili ya wateja na washirika wetu na kupambana dhidi ya udanganyifu kwa kuthibitisha taarifa za mahali zilizowasilishwa na mtumiaji.
  • Maslahi halali
  • Ni lazima ili kutii wajibu wa kisheria (kudhibiti udanganyifu)
  • Idhini
Kitambulisho cha kifaa cha mtumiaji na anwani ya IP, kama vile, mfumo endeshi, mipangilio ya mtumiaji, matumizi yako ya Huduma Kuboresha na kufanya Huduma iwe mahususi kwa mtumiaji, ikijumuisha kutoa na kupendekeza maudhui kulingana na eneo husika la mtumiaji.
  • Maslahi halali
  • Idhini
Taarifa za Kifaa Ili kuelewa vizuri muktadha wa mtumiaji linapofikia suala la uboreshaji wa aplikesheni na kuripoti hitilafu, kukusanya taarifa kwa ajili ya wateja na washirika wetu pamoja na kukusanya data zinazoweza kutumika katika ufumbuzi wa migogoro wakati wa kufanya Kazi zenye malipo.
  • Ili kutimiza mkataba na wewe
  • Maslahi halali
Lugha Ili kuweza kumwasilishia mtumiaji maandishi kwenye aplikesheni katika lugha anayoielewa.
  • Ili kutimiza mkataba na wewe
  • Maslahi halali
Kipimo cha utendaji kwa API Ili kuhakikisha API zote zinazotumiwa na aplikesheni zinafanya kazi ipasavyo ili kutoa huduma bora kwa mtumiaji.
  • Ili kutimiza mkataba na wewe
  • Maslahi halali
Ukusanyaji wa majina ya aplikesheni

 

Ili kupunguza hatari ya udanganyifu kwa kuhakikisha kuwa mtumiaji hatumii aplikesheni inayoweza kubadili taarifa muhimu kwa utendaji kazi wa aplikesheni, m.f. taarifa za mahali kifaa kilipo, saa, n.k. na kukusanya taarifa sahihi kwa ajili ya wateja na washirika wetu.
  • Maslahi halali
  • Ni lazima ili kutii wajibu wa kisheria (kudhibiti udanganyifu)
Hali ya betri Ili kuelewa athari ya aplikesheni yetu kwenye betri ya mtumiaji pamoja na kufuatilia na kutambua udanganyifu.
  • Maslahi halali
  • Ni lazima ili kutii wajibu wa kisheria (kudhibiti udanganyifu)
WiFi na Mtandao wa Simu Ili kuelewa vizuri ubora wa mtandao kwenye kifaa cha mtumiaji, hivyo kusaidia washirika wetu kuboresha mtandao, pamoja na kutoa huduma bora kwa watumiaji kulingana na hali ya mtandao wanaotumia. Maslahi halali
Endapo utajiunga na Pochi ya Premise, pia tunakusanya:

  • Kitambulisho chako cha Mtumiaji wa Premise
  • Kitambulisho chako cha Pochi ya Premise
  • Kitambulisho chako cha mtumiaji wa PrimeTrust
  • Msimbo wa nchi na eneo kwa ajili ya akaunti
  • Jina kamili
  • Tarehe ya kuzaliwa
  • Nambari ya simu
  • Kitambulisho cha mlipa kodi
  • Anwani
  • Picha za kitambulisho kilichotolewa na serikali
  • Picha za nyaraka zinazothibitisha anwani yako ya makazi
  • Picha yako
  • Anwani ya pochi ya sarafu dijitali ya mtoa huduma mwingineyo
Ili kukutambua, kudhibiti, kudumisha na kuendesha huduma pamoja na akaunti yako ya Pochi ya Premise, kupunguza hatari ya udanganyifu, kutii kanuni za serikali, kutimiza matakwa ya “Mjue Mteja Wako”, kurahisisha uchunguzi wa kina kukuhusu, kuwezesha malipo yakufikie, kuthibitisha utambulisho wako na utambulisho wa anwani yoyote ya pochi ya sarafu dijitali ya mtoa huduma mwingineyo na kuwezesha miamala ya sarafu dijitali.

 

 

  • Ili kutimiza mkataba na wewe
  • Maslahi halali
  • Ni lazima ili kutii wajibu wa kisheria (kudhibiti udanganyifu)

 

 

Kwa jumla, tutakusanya aina mbalimbali ya taarifa binafsi zilizotajwa hapo juu ili tuwahudumie watumiaji wetu kwa ubora zaidi na kuzuia watumiaji wadanganyifu kutumia vibaya Huduma zetu, ikiwa ni pamoja na Kazi tunazowalipa watumiaji na kukamilisha miradi kwa ajili ya wateja na washirika. Baadhi au taarifa hizi zote zitatumwa kwenda Premise kupitia Amplitude, ambayo ni kampuni tofauti ya uchanganuzi. Pia, baadhi ya taarifa zilizotajwa hapo juu zinaweza kushirikiwa kwa washirika na wateja wetu.

Ikiwa unataka kupata maelezo zaidi kuhusu taarifa tunazokusanya, yafuatayo ni maelezo machache zaidi:

Taarifa Unazotupatia

Tunakusanya taarifa unazotupatia kwa njia ya moja kwa moja, pamoja na taarifa unazotupatia kupitia matumizi ya akaunti za wahusika wengine. Tunakusanya taarifa wakati unapotengeneza au kubadilisha akaunti yako, unapokamilisha kazi, unapowasiliana na timu yetu ya usaidizi au unapowasiliana nasi kwa namna yoyote ile. Taarifa hii inaweza kujumuisha jina, akaunti ya mitandao ya kijamii, anwani ya barua pepe, nambari ya simu, kitambulisho cha malipo na taarifa nyinginezo unazochagua kutupatia. Aidha, tunakusanya picha, video au rekodi mbalimbali unazowasilisha kwetu, ikiwa ni pamoja na picha, picha za skrini na rekodi za sauti.

Taarifa Tunazokusanya kupitia Matumizi Yako ya Huduma

Unapotumia Huduma, ikiwa ni pamoja na Pochi ya Premise endapo utajiunga ili kuitumia, tunakusanya taarifa kukuhusu katika makundi ya jumla yafuatayo hapo chini:

Taarifa za Mahali: Unapotumia Huduma ili ukamilishe Kazi za Premise, tunakusanya data ya eneo mahususi inayofuatilia eneo la kuanzia na maeneo ya tafiti. Ukiruhusu Huduma ifikie huduma ya mahali kupitia mfumo wa ruhusa unaotumika na mfumo endeshi wa kifaa chako cha mkononi (“jukwaa”), tunaweza pia kukusanya taarifa za eneo mahususi kilipo kifaa chako wakati unatumia aplikesheni yetu au ikiwa inafanya kazi chinichini. Vilevile, tunaweza kukadiria eneo lako kwa kutumia anwani yako ya IP. 

Taarifa za Watu Unaowasiliana nao: Ukiruhusu Huduma itumie rekodi yako ya anwani za simu kupitia mfumo wa ruhusa unaotumika na jukwaa la kifaa chako cha mkononi, tunaweza kufikia na kuhifadhi majina na taarifa za mawasiliano kutoka kwenye rekodi yako ya anwani na kuitumia katika uthibitishaji wa akaunti na pia kualika rafiki na familia pamoja na matumizi mengine yanayofanana.

Taarifa za Betri: Ukiruhusu Huduma ifikie taarifa za betri yako kwenye kifaa chako kupitia mfumo wa ruhusa unaotumika na jukwaa la kifaa chako cha mkononi, tunaweza kufikia na kuhifadhi viwango vya nguvu ya betri yako na hali ya chaji ili kuelewa mazingira ambayo bidhaa zetu zinatumika.

Taarifa ya Miamala: Tunakusanya maelezo ya miamala inayohusiana na matumizi yako ya Huduma ikiwa ni pamoja na maelezo yako ya malipo, mtoa huduma wa malipo unayemtumia, tarehe na saa kazi ilipokamilishwa, kuwasilishwa, kukaguliwa na malipo kufanyika, wakati fedha zilitolewa, kiasi cha fedha kilichotengenezwa, na maelezo mengine yanayohusiana na muamala.

Taarifa za Kifaa: Tunaweza kukusanya taarifa kuhusu kifaa chako cha mkononi, ikiwa ni pamoja na, kwa mfano, modeli ya kifaa chako, mfumo endeshi na toleo, majina ya aplikesheni na faili, lugha unayopendelea, vitambulishi vya kipekee vya kifaa, vitambulishi vya matangazo, nambari tambulishi, taarifa za mwendo wa kifaa na taarifa za mtandao wa simu.
Taarifa ya Kumbukumbu: Unapotumia Huduma, tunakusanya kumbukumbu za seva, ambazo huenda zikajumuisha taarifa kama vile, anwani ya IP ya kifaa, tarehe na muda wa kutumia Huduma, vipengele vya aplikesheni au kurasa zilizotazamwa, matukio ya aplikesheni kuacha kufanya kazi na shughuli nyinginezo za mfumo, aina ya kivinjari, na tovuti au huduma ya mshirika mwingine uliyotumia kabla ya kutumia Huduma. Pia, tunaweza kukusanya shughuli za intaneti na shughuli nyinginezo za mtandaoni, ikijumuisha taarifa za kivinjari na historia, taarifa ya kidakuzi (kulingana na mapendeleo yako ya vidakuzi, ikiwa unayo) na mihuri ya muda.

Taarifa Tunazokusanya Kutoka Vyanzo Vinginevyo

Ukitupatia taarifa za akaunti za wahusika wengine au ukiingia kwenye Huduma kupitia tovuti au huduma nyinginezo, unaelewa kwamba baadhi ya maudhui na/au taarifa katika akaunti hizo (“Taarifa za Akaunti za Wahusika Wengine”) zinaweza kuwasilishwa kwenye akaunti yako ya Premise ikiwa utaidhinisha uwasilishaji huo, na Taarifa za Akaunti za Wahusika Wengine zilizowasilishwa kuja kwenye Huduma zipo chini ya Sera hii. Tunaweza kuchanganya taarifa kutoka kwenye aplikesheni au tovuti hii na taarifa tulizokusanya kutoka kwako kama mtumiaji wa Huduma.

Google, Branch, Leanplum, Amplitude na FullStory pamoja na makampuni mengine yanayofanana na haya ambayo Premise hufanya nayo kazi, yanaweza kukusanya au kupokea taarifa zako zinazokutambulisha kibinafsi, zinazohusu shughuli zako mtandaoni kadri muda unavyosonga na katika tovuti mbalimbali kutoka kwenye Huduma na aplikesheni nyinginezo, na kutumia taarifa hizo ili kuthibitisha kazi na tafiti, kubaini udanganyifu na kutoa huduma za vipimo na matangazo.

Premise inachukulia suala la kuzuia udanganyifu na utii wa sheria kwa uzito mkubwa. Kama sharti la kukidhi vigezo vya kujiandikisha na kukamilisha Kazi kwa kutumia Aplikesheni, Premise inaweza kufanya uchunguzi wa kina kukuhusu, kama itavyoona inafaa na kwa busara zake.

Maelezo Muhimu Kuhusu Ruhusa za Jukwaa

Majukwaa ya vifaa vya mkononi yamefafanua aina fulani ya data za kifaa ambazo aplikesheni haziwezi kufikia bila ruhusa yako. Majukwaa haya yana mifumo tofauti ya ruhusa kwa ajili ya kupata ridhaa yako. Vifaa vya Android vitakuarifu juu ya ruhusa ambazo aplikesheni ya Premise inahitaji kabla ya kutumia aplikesheni kwa mara ya kwanza, na matumizi yako ya aplikesheni huashiria idhini yako.


MATUMIZI YA TAARIFA

Tunaweza kutumia taarifa tunazokusanya kukuhusu, ikijumuisha picha, video, rekodi mbalimbali, picha na picha za skrini, kufanya yafuatayo:

    • Kutoa, kudumisha, na kuboresha Huduma, ikiwa ni pamoja na Pochi ya Premise endapo utajiunga ili kuitumia, ikijumuisha kwa mfano, kuwezesha malipo, kukupatia huduma na bidhaa unazoomba (na kutuma taarifa zinazohusiana), kusanidi vipengele vipya, kutoa msaada kwa watumiaji, kuthibitisha watumiaji na kutuma taarifa mpya kuhusu bidhaa na ujumbe wetu wa kiutawala;
    • Kutekeleza shughuli za ndani ya kampuni, ikijumuisha, kwa mfano, kuzuia udanganyifu na matumizi mabaya ya Huduma, ikiwa ni pamoja na Pochi ya Premise endapo utajiunga ili kuitumia, kutatua hitilafu za aplikesheni na matatizo ya utendaji kazi; kufanya uchanganuzi, upimaji na utafiti wa data; na kusimamia na kuchanganua mwenendo wa matumizi na shughuli;
    • Kuwapatia wateja na washirika wetu uchanganuzi wa data, ikiwa ni pamoja na uchanganuzi wa kiotomatiki unaowezeshwa na akili bandia;
    • Kutuma au kuwezesha mawasiliano kati yako na mfumo wetu wa ndani wa usaidizi, kama vile, arifa muhimu zinazohusu kikundi mahususi cha watumiaji;
    • Kukutumia mawasiliano tunayodhani yatakuwa na manufaa kwako, ikiwa ni pamoja na taarifa kuhusu bidhaa, huduma, promosheni, habari, matukio ya Premise na kampuni nyinginezo, pale inaporuhusiwa na kwa mujibu wa sheria zinazotumika katika eneo lako; na kuchakata ushiriki katika shindano, bahati nasibu, au ushiriki mwingine katika promosheni na kutimiza zawadi zozote zinazohusiana; na
    • Kuboresha na kufanya Huduma kuwa mahususi kwako, ikiwa ni pamoja na Pochi ya Premise endapo utajiunga ili kuitumia, ikijumuisha kutoa au kupendekeza vipengele, maudhui, mialiko na matangazo. 

Msingi wa kisheria wa sisi kutumia taarifa zako binafsi kwa madhumuni ya kimkataba au kisheria tunapozihitaji ili kutoa Huduma, ikiwa ni pamoja na Pochi ya Premise endapo utajiunga ili kuitumia, au kuendesha tovuti au kwa ajili ya maslahi yetu halali, ikijumuisha biashara yetu kiujumla na shughuli za matangazo, kwa ajili ya uchunguzi au sababu za migogoro na madhumuni ya promosheni. Pale tunapotegemea maslahi halali kama msingi wa kuchakata taarifa zako binafsi, chini ya sheria husika unaweza kuwa na haki ya kupinga uchakataji huu.

KUSHIRIKI TAARIFA

Tunaweza kushiriki au kuuza taarifa tunazokusanya kukuhusu, kama vile, picha, video, rekodi mbalimbali, picha na picha za skrini, kama ilivyoelezwa katika Sera hii ya Faragha (ikiwa ni pamoja na Pochi ya Premise endapo utajiunga ili kuitumia) uchanganuzi unaotokana na taarifa hiyo (ikijumuisha uchanganuzi wa kiotomatiki unaotumia akili bandia), au kama ilivyoelezwa wakati wa kukusanya au kushiriki taarifa, ikijumuisha yafuatayo:

    • Pamoja na washirika wanaotoa huduma au kufanya ukusanyaji na/au uchakataji wa data kwa niaba yetu, au kwa madhumuni ya kuweka pamoja data na/au madhumuni ya uhamishaji;
    • Pamoja na wateja wanaoifuata Premise kwa ajili ya kukusanya data, picha, rekodi mbalimbali na video, ikijumuisha picha, picha za skrini na rekodi za sauti, ndani ya maeneo tofauti duniani kwa ajili ya matumizi yao au matumizi ya wateja wao, ndani au nje. Hii inamaanisha taarifa na picha, video, rekodi mbalimbali, picha na picha za skrini unazotupatia huenda zikachapishwa na wahusika wengine (wateja wetu au wateja wao) kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa mengineyo;
    • Pamoja na makampuni mengine, washauri, washauri wa kibiashara, washirika wa masoko, wakaguzi wa mahesabu, washauri wenye utaalamu kama vile, washauri wa fedha au washauri wa kisheria na watoa huduma wengine wanaohitaji kupata taarifa hizo ili kufanya kazi kwa niaba yetu au kutupatia ushauri au huduma;
    • Kulingana na ombi la kupata taarifa kutoka kwa mamlaka iliyoidhinishwa kufanya hivyo, ikiwa tunaamini kwamba kufichua taarifa hizo ni kwa mujibu wa sheria husika, au inahitajika kupitia kanuni, au mchakato wowote wa kisheria kama vile, hati ya kuitwa mahakamani, hati ya upekuzi, amri za mahakama;
    • Ili kuanzisha au kutumia haki za kisheria, au kujitetea dhidi ya madai ya kisheria;
    • Ili kuchunguza, kuzuia, au kuchukua hatua dhidi ya madai au shughuli iliyo kinyume cha sheria, ukiukaji wa Masharti ya Huduma, au inavyotakiwa na sheria;
    • Ili kutii sheria husika, ikijumuisha sheria zinazohusiana na kodi; 
    • Ili kuendesha promosheni au utafiti; 
    • Pamoja na maafisa wanaotekeleza sheria, mamlaka za serikali au watu wengine ikiwa tunaamini vitendo vyako haviendani na Masharti ya Huduma au sera nyinginezo husika, au kulinda haki, mali, au usalama wa Premise au wengine;
    • Kuhusiana na, au wakati wa mazungumzo ya, muungano wowote wa kibiashara, uuzaji wa mali za kampuni, uimarishaji au urekebishaji, ufadhili, au ununuzi wa sehemu au biashara yetu yote na kampuni nyingineyo;
    • Ikiwa tumekujulisha (ikiwa ni pamoja na kukutumia notisi kwenye aplikesheni au kwenye maelezo ya kazi husika) na, inapohitajika, ukaruhusu kushiriki taarifa hiyo; na
    • Kwa fomu ya jumla na/au isiyoonyesha utambulisho na ambayo haiwezi kutumika kukutambua.

Uchanganuzi na Huduma za Matangazo Zinazotolewa na Wengine

Tunaweza kuruhusu wengine watoe huduma za uchanganuzi na upimaji wa kiwango cha matumizi kwa ajili yetu, kuonyesha matangazo mtandaoni kwa niaba yetu na kufuatilia pamoja na kuripoti kuhusu utendaji wa matangazo hayo. Mashirika haya yanaweza kutumia vidakuzi, bikoni za mtandao, SDK na teknolojia nyinginezo ili kutambua kifaa chako wakati unatumia Huduma, pia wakati unapotembelea tovuti na huduma nyinginezo za mtandaoni.

MACHAGUO YAKO

Taarifa za Akaunti

Unaweza kurekebisha au kufuta taarifa zako za akaunti wakati wowote kwa kuingia kwenye akaunti yako katika aplikesheni. Tafadhali kumbuka, katika hali fulani tunaweza kubaki na baadhi ya taarifa za kukuhusu kama inavyohitajika kisheria au kwa madhumuni halali ya kibiashara kwa muda unaoruhusiwa kisheria. Kwa mfano, ikiwa una deni au malimbikizo kwenye akaunti yako au endapo tutaamini umefanya udanganyifu au kukiuka Sera zetu za Matumizi, tunaweza kuhitaji kutatua suala hilo kabla ya kufunga akaunti yako.

Haki za Kufikia

Premise itatii maombi ya mtu binafsi yanayohusu kufikia, kurekebisha, na/au kufunga akaunti ya mtumiaji au kufuta taarifa binafsi za mtumiaji kwa mujibu wa sheria zinazotumika.

Taarifa za Mahali

Huduma, ikiwa ni pamoja na Pochi ya Premise endapo utajiunga ili kuitumia, huomba ruhusa ili ikusanye taarifa mahususi za mahali kutoka kwenye kifaa chako kupitia mfumo wa ruhusa unaotumiwa na mfumo endeshi wa kifaa chako cha mkononi. Kuzuia ukusanyaji wa taarifa hii kutapunguza uwezo wako wa kufikia Huduma. Hata hivyo, kuzuia uwezo wa Huduma kukusanya taarifa mahususi ya mahali kutoka kwenye kifaa chako hakutazuia uwezo wetu wa kukusanya taarifa za mahali ulipo kupitia anwani yako ya IP.

SEHEMU YA NNE – HAKI ZAKO ZA FARAGHA ZA CALIFORNIA NA MAJIMBO MENGINE

Ibara zifuatazo zitatumika kama inavyotakiwa kisheria kwa Wachangiaji, Wageni na Wateja ambao ni wakazi wa jimbo la California na majimbo mengine, pale inapofaa (kama vile, Colorado, Connecticut, Nevada, Utah, Virginia au, kwa hapo baadaye chini ya sheria mpya zitakazopitishwa kwenye majimbo ya Delaware, Indiana, Iowa, Montana, Oregon, Tennessee na Texas). Ibara hizi hazitumiki kwenye taarifa binafsi ambazo hazina ulinzi chini ya Sheria ya Haki ya Faragha ya California ya 2020 (“CPRA”) au sheria nyinginezo za jimbo zinazotumika.

Haki ya Kufahamu. Unaweza kuomba tukupatie orodha ya aina za taarifa binafsi tulizokusanya kukuhusu ndani ya kipindi mahususi cha muda (kinachodhibitiwa kisheria), aina ya vyanzo ambavyo taarifa hizo zilikusanywa, madhumuni ya kibiashara ya kukusanya au kuuza taarifa hizo na aina ya wahusika wengine ambao tulifichua au kuwauzia taarifa hizo. Isitoshe, unaweza kuomba tukupatie nakala ya aina fulani ya taarifa binafsi tulizokusanya kukuhusu ndani ya kipindi mahususi cha muda (kinachodhibitiwa kisheria). Wakazi wa jimbo la California wanaweza kutuma maombi mawili ya kufahamu ndani ya kipindi cha miezi 12, kwa mujibu wa vikomo vilivyoelezwa kwenye sheria. Majimbo mengine yanaukomo pia. Ili ufahamu orodha ya aina za jumla za taarifa tulizokusanya na kushiriki ndani ya kipindi cha miezi 12, soma ibara za Sera ya Faragha zilizopo juu. 

Haki ya kusahihisha. Unaweza kuomba kusahihishwa kwa taarifa zozote binasi zisizosahihi tulizokusanya kukuhusu.

Haki ya Kufuta. Unaweza kuomba tufute taarifa zozote binafsi ambazo tumekusanya kutoka kwako, hii haijumuishi taarifa ambazo tunaruhusiwa kisheria kubaki nazo. Tunapojibu ombi lako la kufuta taarifa, tutakupatia ufafanuzi wa aina ya taarifa tulizobakiza (kama zitakuwepo) na kwa nini. Yaliyotangulia hayatumiki kwenye taarifa binafsi ambazo hazijapatiwa ulinzi kisheria.

Jinsi ya Kutuma Ombi la Kufahamu, Kusahihisha au Kufuta. Unaweza kutuma ombi la kufahamu, kusahihisha au kufuta taarifa kupitia aplikesheni au kwa kututumia barua pepe kwenda: [email protected]. Unapotuma ombi, tutachukua hatua za kuthibitisha utambulisho wako kabla ya kukujibu. Tunachukua hatua hii ili kulinda taarifa zako. Tutakuomba utupatie anwani yako ya barua pepe. Ukiwa una akaunti nasi, anwani hiyo lazima ifanane na ile iliyounganishwa na akaunti yako. 

Wakala Aliyeidhinishwa. Unaweza kumteua wakala aliyeidhinishwa afanye maombi kwa niaba yako katika baadhi ya majimbo. Tutahitaji uthibitisho wa kwamba umemuidhinisha wakala huyo. Isipokuwa kama sheria itahitaji vinginevyo, wakala uliyemuidhinisha lazima atupatie taarifa zako za mawasiliano. Tutawasiliana nawe ili kuthibitisha kwamba umemuidhinisha wakala huyo. Utakapothibitisha, tutajibu mara moja ombi la haki.

Hakuna Kuuza au Kushiriki Taarifa Binafsi bila Idhini. Hatuuzi wala kushiriki taarifa binafsi za Wageni au Wateja. Tunaweza kuuza au kushiriki taarifa binafsi, ikiwa ni pamoja na picha, video, rekodi mbalimbali, picha na picha za skrini za Wachangiaji kwa wahusika wengine kama ilivyoelezwa katika Sera hii ya Faragha.

Kutokubaguliwa. Una haki ya kutokubaguliwa unapotumia haki zako.

Haki ya Wakazi wa California ya Kuomba Taarifa Kuhusu Ufichuzi wa Taarifa kwa Wahusika Wengine Kwa Madhumuni yao ya Mauzo ya Moja kwa Moja. Unaweza kuomba taarifa kuhusu ufichuzi wa taarifa binafsi kwa wahusika wengine au kampuni washirika kwa madhumuni ya mauzo ya moja kwa moja. Ili kutuma ombi hilo, tafadhali tutumie barua pepe kwenda: [email protected]. Tafadhali fahamu kwamba inaweza kutuchukua hadi siku 30 kulifanyia kazi ombi lako. Unaweza kututumia ombi hili mara moja tu kwa mwaka.